Kitabu hiki kinaturudisha katika kipindi cha kusisimuwa cha miaka ya vita baridi, kipindi ambacho, sambamba na kipindi cha leo, madola ya kibeberu yamekuwa yakifanya njama za kubadilisha serikali zilizokuwepo na kuziweka madarakani zile zenye kufuata amri. Kwa kutumia kumbukumbu za picha za Johari, nyaraka za siri za Marekani na Uingereza, pamoja na mahojiano ya kina, kitabu kinatowa uchambuzi juu ya nafasi na satwa ya Chama cha Umma Party nchini Zanzibar na kiongozi wake mwenye upeo mkubwa wa mambo, Mwanamapinduzi mfuasi wa Itikadi ya Karl Marx, Abdulrahman Mohamed Babu. Kwa kuangalia kwa njia ya uwiano wa mifano inayokwenda sambamba ya wahka wa Marekani kuhusu Uchina ya Kikomunisti katika miaka ya 1960 na woga walionao hivi sasa kuhusu ushawishi wa Uchina, kitabu kinatafakari juu ya mivutano mipya iliyopo katika kupigania rasilmali za Afrika, kuundwa kwa kikosi cha AFRICOM, na jinsi Wanasiasa wa Afrika Mashariki wanavyoshiriki katika kuimarisha udhibiti wa Marekani katika nchi zao, na “Vita dhidi ya Ugaidi” katika ukanda wa Afrika Mashariki hivi sasa.

Now available from Mkuki Na Nyota Publishers, Tanzania: http://www.mkukinanyota.com

Share this out
  • ISBN print: ISBN-13: 978-0995222328
  • Publication date: 09/22/2016
  • Page count: 204
  • Binding type: Paperback
  • Trim size: 6x9
  • Language: Swahili
  • Colour: B&W
  • Print book available from: Price includes shipping
  • E-pub available from: Available from Daraja Press
  • Kindle version available on Amazon: Available from Daraja Press

Clear

Kitabu hiki kinaturudisha katika kipindi cha kusisimuwa cha miaka ya vita baridi, kipindi ambacho, sambamba na kipindi cha leo, madola ya kibeberu yamekuwa yakifanya njama za kubadilisha serikali zilizokuwepo na kuziweka madarakani zile zenye kufuata amri. Kwa kutumia kumbukumbu za picha za Johari, nyaraka za siri za Marekani na Uingereza, pamoja na mahojiano ya kina, kitabu kinatowa uchambuzi juu ya nafasi na satwa ya Chama cha Umma Party nchini Zanzibar na kiongozi wake mwenye upeo mkubwa wa mambo, Mwanamapinduzi mfuasi wa Itikadi ya Karl Marx, Abdulrahman Mohamed Babu. Kwa kuangalia kwa njia ya uwiano wa mifano inayokwenda sambamba ya wahka wa Marekani kuhusu Uchina ya Kikomunisti katika miaka ya 1960 na woga walionao hivi sasa kuhusu ushawishi wa Uchina, kitabu kinatafakari juu ya mivutano mipya iliyopo katika kupigania rasilmali za Afrika, kuundwa kwa kikosi cha AFRICOM, na jinsi Wanasiasa wa Afrika Mashariki wanavyoshiriki katika kuimarisha udhibiti wa Marekani katika nchi zao, na “Vita dhidi ya Ugaidi” katika ukanda wa Afrika Mashariki hivi sasa.

Unaweza kusoma kitabu hiki mtandaoni bila malipo.

Amrit Wilson amechota kutoka vyanzo mbalimbali maelezo yaliyomuwezesha kuandika kuhusu Zanzibar ya nyakati za sasa. Kitabu hiki kinastahiki kusomwa na walio wengi. MAHMOOD MAMDANI, Profesa wa Masuala ya Utawala katika Chuo Kikuu cha Herbert Lehman, na Profesa wa Anthropologia katika Chuo Kikuu cha Columbia.

Amrit Wilson anafanya uchambuzi wa kina wenye kugusa hisia za msomaji kuhusu mapambano halisi na thabit dhidi ya ukoloni mamboleo kama vile ambavyo yamekuwa yakijitokeza na kuendeshwa nchini Zanzibar na Tanzania. Kwa kutumia nyaraka ambazo hapo awali zilikuwa hazipatikani, ameweza kumvuta msomaji na kumpeleka katika harakati za miaka ya 1960 ambazo zingeliweza kuleta mabadiliko ya maana ya kimapinduzi nchini Zanzibar, na yumkini pia katika sehemu nyengine za Afrika Mashariki, kama harakati hizo zisingelitekwa nyara … Baadhi ya sehemu za maelezo ya kitabu yanatowa taswira na hisia zinazomfanya msomaji kujihisi yumo kuwemo katika kusoma riwaya !

BILL FLETCHER, JR.. mwandishi na mwanaharakati, mwandishi-mwenza wa Solidarity Divided na pia mwandishi-mwenza wa Claim No Easy Victories: The Legacy of Amilcar Cabral

AMRIT WILSON ni mwandishi na mwanaharakati. Miongoni mwa vitabu vyake ni pamoja na Dreams, Questions, Struggles: South Asian Women in Britain (Pluto Press, 2006), “Ndoto, Maswali, Mapambano: Wanawake wa Asia ya Kusini Ulaya ya Uingereza” na US Foreign Policy and Revolution: The Creation of Tanzania (Pluto Press, 1989) “Sera ya Mambo ya Nje ya Marekani na Mapinduzi: Kuundwa kwa Tanzania”

You may also like…